Wednesday, June 14, 2017

HOW TO ORGANISE A SMALL PARTY..

Kabla ya kuandaa party inatakiwa kwanza uweze kufikiria jinsi gani utawafanya wageni wako wajisikie wenye  furaha katika moyo na waone party yako ni ya tofauti zaidi, kikubwa ni ubunifu wa kufanya  party ichangamke na wageni wajisikie raha…"its all about happiness and enjoying the moment".

  • Cha kwanza ni vizuri kujua utaandaa sherehe ya aina gani; kama itakua ya watoto, ya kidini, ya vijana au wazee. Na pia ukishajua ni watu wa aina gani hivyo inakua rahisi kujua itafanyika sehemu gani kama ni nyumbani, by the poolside, beach au kwenye hall.
  • Baaada ya kuamua hayo yote, sasa unaweza kuchagua  theme ambayo itaendana na sherehe yako. Kuna theme mbali mbali inategemea unataka theme gani kwajili ya sherehe yako. Kuna Hollywood old school party, Champagne and desert party na nyingine nyingi tofauti kulingana na  ubunifu wako.  Unaweza ukabuni  jina upendalo kutegemeana na decorations zako, mavazi, vyakula na vinywaji  kutokana na party upendayo.

Leo nita share na nyie party niliomuandalia mdogo wangu, niliita “Julies cup cakes and Barbeque royal Party”. Ntaanza kwa kuelezea theme ya bbq party, kabla ya kufanya bbq inabidi kuangalia hali ya hewa (weather) ya siku hiyo mara nyingi inaendana na wakati wa summer au pale jua linapotoka inapendeza ukiandaa wakati hakuna mvua.
Bbq Party ni kuhusu nyama choma mfano mbuzi, kuku, beef, sausages, samaki, pork/kitimoto na burgers. Pia usisahau kuna ambao hawatakula nyama hao wawekee vegetable-bbq kama mahindi ya kuchoma,ndizi mzuzu, viazi vitamu vya kuchoma.


Wageni wako watakuja kwenye sherehe na matarajio ya kula, kushiba na kuenjoy nyama choma kwahiyo hakikisha una nyama ya kutosha kulingana na wageni uliowaalika na nyama yako inafanyiwa marination usiku mmoja kabla ya sherehe.
Unaweza marinate nyama yako kwa kutumia classic sauces na spices.  Ili nyama yako iweze kuiva taratibu na spice kukolea vizuri, unashauriwa kufanya marination usiku mmoja kabla ya party. Pia tayarisha sauces za kusevia nyama choma.

Unaweza kutayarisha pia cool drinks na ice na waweza kutengeneza cocktail drinks pia.
Ni vizuri kuandaa corner ya chai na coffee, maana kuna wageni wako wengine watapendelea kupata chai na coffee. Hakikisha unasahani za kutosha za disposable zenye rangi ya kuvutia ya summer.


hakikisha una cutlery za kutosha; vijiko na uma na visu. kuhusu bbq kumbuka kwamba wageni hawata kua na muda wa kusubiri chakula, hakikisha nyama zinachomwa mapema  kabla ya wageni kuwasili ili wakija wanakutana na harufu nzuri na wakikaa kidogo wanaanza kuseviwa.




SPECIAL THANKS TO MAMA KAI KAI for the great post .....

No comments:

Post a Comment